Ruka hadi kwenye maudhui makuu

MAXIMO, MART NOOIJ WANUNIANA

KOCHA mkuu wa timu ya taifa, Taifa Stars Mholanzi Mart Nooij na Mbrazil Marcio Maximo anayeinoa Yanga wameingia vitani kila mmoja akitaka kuona taifa lake linaibuka mbabe wa soka duniani, Brazil na Uholanzi zipo katika kombe la dunia linalofanyika nchini Brazil.

Huku timu hizo zote mbili zikifanikiwa kuingia nusu fainali, wakati kesho Brazil ikicheza na Ujerumani, Uholanzi itakuwa na shughuri pevu itakaposhuka uwanjani kukabiliana vikali na Argentina siku inayofuata yaani Jumatano.


Maximo raia wa Brazil akiwahamasisha mashabiki wa Yanga kuishangilia Brazil, Nooij naye amekuwa akiwahamasisha mashabiki wa Tanzania kuipenda Uholanzi, makocha hao sasa wanaingia katika vita kubwa ambapo mshindi ni yule ambaye taifa lake litafanya kweli na kuchukua kombe hilo lililoachwa na watetezi Hispania ambao waliondolewa katika hatua za mwanzo.

Maximo haivi chungu kimoja na Nooij kwa sababu ya utaifa

Haijulikani nani ataibuka mbabe katika michuano hiyo mikubwa kuliko yote ulimwenguni lakini kila timu imepewa nafasi ya kushinda, Brazil kikosi chake hakionyeshi soka safi kiasi kwamba kupewa nafasi finyu kuifunga Ujerumani lakini haitabriki kutokana na kushinda mechi zake ngumu.

BNrazil iliifunga Colombia timu ambayo inacheza soka safi na la kupendeza, Uholanzi nayo imeonyesha umahiri wa hali ya juu kiasi kwamba mashabiki wa soka wanaipa nafasi kubwa kubeba ndoo huku Argentina ikipewa nafasi finyu mbele ya Wadachi hao wanaouungwa mkono na kocha wa Stars ambaye ni Mholanzi

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetoa orodha ya viwango vya ubora wa klabu barani, Simba ikiendelea kuwa juu ya klabu nyingine za Tanzania, nafasi ya tano. Orodha hiyo imetoka leo kuelekea droo ya hatua za awali za michuano ya klabu Afrika ambayo kwa mara ya kwanza kihistoria itafanyika nchini katika studio za Azam Tv, Tabata Jijini Dar es Salaam. Yanga ambayo kama Simba itashiriki Ligi ya Mabingwa — yenyewe inashika nafasi ya 12, wakati timu nyingine katika orodha hiyo ni Namungo FC wanaoshika nafasi ya mwisho, ya 75 kwa pamoja na Salitas FC ya Burkina Faso, Ahli Benghazi ya Libya na NAPSA Stars ya Zambia. Kwa msimu ujao mbali na Simba na Yanga kushiriki Ligi ya Mabingwa, Azam FC na Singida Black Stars zitashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

Miongoni mwa viungo wa pembeni wanaofanya vizuri ni Benodict Khalfan Ngassa ambaye amekuwa akifanya vizuri. Ngassa ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Pamba Jiji na Simba SC, Khalfan Ngassa, pia ni mdogo wa kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Simba na Azam, Mrisho Ngassa anatajwa ni mmoja kati ya wachezaji wanaotazamiwa kufanya makubwa siku za usoni. Mambo Uwanjani Blog itawaletea Makala maalum ya kiungo huyo hatari ambaye ndoto zake ni kufuata nyayo za kaka yake Mrisho Ngassa. Beno Ngassa

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe