DUDUBAYA AFUKUZWA NYUMBANI KWA MPENZI WAKE KWA TUHUMA ZA UBAKAJI

Mwanamke mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Mary "Mama wa Kinyakyusa" amedai kuwa eti amekua akiishi kinyumba na msanii wa Bongo Flava Dudubaya kwa muda mrefu lakini hivi karibuni eti alimfukuza nyumbani msanii huyo kutokana na kukithiri kwa vitendo vyake viovu ikiwemo ubakaji na unyanyasaji, hayo aliyasema kupitia HekaHeka ya Leo Tena (Cloudsfm)

Mama wa Kinyakyusa anadai alikua anamnyima unyumba Bwana ake wa zamani (DuduBaya) kwa sababu eti Dudu akishalewa pombe anakua mtata matusi kwa wingi na eti DuduBaya anauwezo wa kuishi Bar siku tatu mfululizo huku akitandika kilauri.


Na akaanza tabia ya kumwingilia kinguvu mara kwa mara dada huyu, alipoona mateso yanazidi akamfukuza Dudu hapo nyumbani kwani hata kodi ya pango eti anailipa yeye Mwanamke.

Mary alichukua vitu vyote alivyowahi kumnunulia Dudubaya ikiwemo jeans, fulana na zagazaga nyingine, baada ya tukio hilo Dudu akawa anamfanyia vurugu nyumbani kwake hadi Mary akaamua kwenda polisi kumshtaki.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA