CHEGE: WAUWE NI VIDEO BORA LAKINI WATANZANIA WAMEROGWA

Chege na Temba mwanzoni mwa mwezi huu wali release video kali ya Wauwe ambayo director Adam Juma alitumia red camera – camera ambayo inasemekana kuwa ni bora katika kupata picha bora za video.Sasa ndani ya Burudani Chegge amefunguka kuwa bajeti ya video hiyo ilikuwa kubwa kidogo zaidi ya Milioni 10 kutokana na tathmini aliyopewa na Meneja wake, Saidi Fela.

Pia Chegge alifunguka kuwa anaamini wauwe ni video kali sana, kwa video ambazo zimefanywa ndani ya nchi, hadhani kama kuna video ya kuweza kuifananisha nayo.


"Mi naamini wauwe ni video kali sana lakini kutokana na watanzania wanalogeka kirahisi sana, yaani wamekremishwa sasa hivi video kali mpaka ukashuti nje, kitu ambacho mi sitaki kukifanya, ingawa nimepata nafasi ya kufanya video nje, sasa hivi Chegge na Temba tunaenda kufanya kwa sababu ni nafasi ambayo tumepewa huwezi kukataa lakini kimaamuzi mimi sitaki kufanya hivyo" alisema.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA