IRENE UWOYA, JAGUAR WADAIWA KUKUTANA FARAGHA NAIROBI, MINONG'ONO YAANZA!
Chanzo kimoja kilicho karibu na Uwoya kikizungumza na Swahiliworldplanet kimesema kuwa wawili hao kuna deal wanafikiria kufanya pamoja lakini hana uhakika mpaka sasa ni deal gani "Uwoya na Jaguar wamekutana faragha kuna issue zao wana-talk ila sijui ni deal gani hizo, nitakupa updates" kilisema chanzo hicho jana
Hata hivyo chanzo kingine kutoka Kenya kimesema kuwa kimewaona Uwoya na Jaguar katika hotel moja jijini Nairobi wakiwa katika mikao ya kimahaba a.k.a zero distance " Hi, I have seen Irene Uwoya with Jaguar in a hotel in Nairobi they looked like an item, hawa celebs sio predicted" kilisema chanzo hicho
SWP imejaribu kumsaka Uwoya lakini namba yake haikupatikana, hata hivyo juzi Uwoya aliweka picha akiwa Julius Nyerere International Airport akisema anaenda Nairobi ingawa hakuweka wazi kama anaenda kikazi au lah ! . Tunamsaka Uwoya ili afunguke mwenyewe live