Djokovic ndiye bingwa wa Wimbledon
Mchezaji tenis wa Serbia Novak Djokovic ndiye bingwa wa mwaka huu wa kombe la Wimbledon.
Djokovic alimlaza Mswisi Rodger Federer seti
tatu kwa mbili za alama 6-7 (7/9), 6-4, 7-6 (7/4), 5-7, 6-4 katika
fainali hizo za wanaume..
Bingwa huyo wa mwaka wa 2011
alitamatisha msururu wa kushindwa kwa mataji makuu ya Grand Slam
alipoandikisha taji lake kuu la 7 .
Mchezji huyo mwenye umri wa miaka 27
alishangilia ushindi huo wa kihistoria kwa kupigasijida katikati ya
uwanja wa kati huko wimbledon na kutafuna nyasi asijue aliwahi vipi
kumkomesha federer ambaye alikuwa anatafuta taji lake la nane na la
kuvuweka rekodi mpya.
Iwapo angeshinda Federer angekuwa ndiye mchezaji mkongwe zaidi kuwahi kutaa ubingwa huo akiwa na umri wa miaka 32 .
Rekodi ya sasa inashikiliwa na Pete Sampras ambaye ameshinda mataji saba sawa na Federer.