DEMBA BA KWENDA BESITKAS KWA PAUNI MILIONI 8

Mshambuliaji wa Chelsea Demba Ba anakaribia kuhamia klabu ya Besitkas ya Uturuki baada ya klabu hizo mbili kukubaliana.

Licha ya kupachika mabao muhimu dhidi ya Liverpool, Swansea na Paris St-Germain mwishoni mwa msimu uliopita, mshambuliaji huyo kutoka Senegal hakuweza kujihakikishia namba chini ya Jose Mourinho.

Kuwasili kwa Diego Costa kwa pauni milioni 32 kutoka Atletico Madrid na uwezekano wa Romelu Lukaku kurejea katika kikosi, Ba hatokuwa na nafasi kubwa ya kucheza.

"Mazungumzo bado yanaendelea. Chelsea walitaka pauni milioni 10, lakini tumekubaliana bei nzuri. Tutawaambia waandishi wa habari mkataba utakapofikiwa." amesema Fikret Orman, rais wa Besitkas.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA