NEYMAR AKESHA AKILIA KWA KIPIGO CHA MABAO 7-1, ADAI YEYE NI MBRAZIL DAMU
NYOTA wa Brazil, Neymar alishindwa kuyazuia machozi wakati akisema ilibaki kidogo tu apooze.
Neymar, alifanya Mkutano wa kwanza na Waandishi wa Habari baada ya kutoka hospitali alipokuwa amelazwa baada ya kuumizwa mgongo katika mechi ya Robo Fainali ya Kombe la Dunia Brazil ikiitoa Colombia.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 pia amesema kwamba beki wa Colombia, Juan Zuniga amempigia simu kumuomba msamaha kwa kumpiga kwa goti mgongoni kwenye mechi hiyo.
"Zuniga alinipigia simu siku chache baadaye kuniomba msamaha na kuniambia kwamba hakudhamiria kuniumiza," amesema Neymar.
"Nimeukubali msamaha huu, lakini siwezi kulichukulia lile kama tukio la kawaida. Siwezi hata kusema lilikuwa tukio la makusudi, lakini kila mmoja anafahamu haikuwa kawaida.
Namna alivyokuja, nyuma yangu, nisingeweza kujitetea.
"Namshukuru Mungu kanisaidia, kwa sababu kama pigo lile lingezama ndani kwa inch chache, ningeweza kupooza,"amesema Neymar huku akibubujikwa na machozi.
Neymar amesema hajui mini tatizo hadi Brazil ikafungwa 7-1 katika Nusu Fainali na Ujerumani. "Kilichotokea hakikutarajiwa. Lakini hata walipokuwa nyuma kwa 6-0, 7-0, hawakukata tamaa, waliendelea kukimbia, kuendelea kujaribu.
Sioni aibu kuwa Mbrazil, sioni aibu kuwa sehemu ya timu hii. Ninajivunia kila mmoja katika wachezaji wenzangu,"amesema.