WEBB KUCHEZESHA FAINALI KOMBE LA DUNIA
Referii muingereza
anayefahamika kwa ukakamavu wake Howard Webb ni miongoni mwa waamuzi 15
walioteuliwa kusalia Brazil kushiriki mechi zilizosalia za kombe la
dunia.
Webb pamoja na wasaidizi wake Mike Mullarkey na Darren Cann wamekwisha amua mechi mbili za kombe la dunia huko Brazil.
Webb alijiimarisha wasifu wake mwaka wa 2010 alipoamua mechi ya fainali ya kombe la dunia baina ya uhispania na Uholanzi nchini Afrika Kusini .
Na baada ya kutizama kanda za video Webb alikiiri kuwa alistahili kumwonesha mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United kadi nyekundu .
Refarii mmoja pekee kutoka Brazili, Sandro Ricci ndiye aliyesalia kuamua mechi zilizosalia za nusu fainali fainali na mechi ya kuamua mshindi wa tatu.
Mbali na Brazili Argentina, Ujerumani na Uholanzi ndiyo mataifa yaliyosalia katika kipute hicho.
Mechi hiyo itachezwa Jumanne .
Rodriguez ndiye refarii ambaye alikosa kumuona mshambulizi wa Uruguay Luiz Suarez akimng'ata mlinzi wa Italia Giorgio Chiellini.