TUTAISHINDA UJERUMANI- SCORARI

Mlinzi wa Brazil Thiago Silva hatocheza katika mechi ya kwanza ya nusu fainali dhidi ya Ujerumani Jumanne .Hii ni baada ya juhudi za shirika la soka la Brazil kukata rufaa kwa shirikisho la soka duniani FIFA kutaka kadi ya pili ya njano iliyompelekea kupigwa marufuku mechi hiyo muhimu kuambulia patupu.
Fifa imepuzilia mbali ombi la BFA la kuitaka ibatilishe kadi ya njano ambayo imemlazimu kocha Luiz Felipe Scolari kutafuta mlinzi mbadala kuziba pengo la nahodha huyo.


Thiago alionesha kadi yake ya pili timu hiyo ilipoilaza Colombia Ijumaa iliyopita.
Kauli hiyo ni pigo kwa wenyeji hao ambao tayari wamempoteza Mshambuli machachari Neymar ambaye alijeruhiwa uti wa mgongo.
FIFA imekataa kubatilisha kadi ya Silva
Kocha wa Brazil Scolari anapanga kutumia Willian kuziba pengo la Neymar.
Scolari amesema kuwa Brazil itajitahidi dhidi ya Ujerumani licha ya kumkosa Neymar ambaye alikuwa ameifungia mabao manne.

Kwa upande wake kocha wa Ujerumani Joachim Low amesema kuwa Wabrazil ni wakakamavu na mara nyingi wanacheza kwa nguvu.

Low amemtaka refarii wa Mexico Marco Antonio Rodriguez kutolegeza kamba dhidi ya wenyeji hao kutokana na nyendo zao .

Timu hizo zitafungua kampeini yao katika mechi ya kwanza ya nusu fainali huko Belo Horizonte.
Matumaini ya wenyeji kutwaa ubingwa wa dunia yameimarika baada ya timu hiyo kufuzu kwa nusu fainali .
Brazil kukwaruzana na Ujerumani
Tiketi ya Mechi hiyo dhidi ya Ujerumani tayari zimeuzwa zote uwanja wa Estadio Mineirao ikitarajiwa kujaa furifuri na zaidi ya mashabiki elfu 62,000.

Mara ya mwisho timu hizo zilipokutana Brazil iliibuka washindi wa 2-0 mwaka wa 2002 katika kombe la dunia huko Japan.

Ujerumani kwa upande wao wanaingia katika mechi hii ikiwa ndiyo mara ya nne kwao kushiriki katika nusu fainali japo hawafuzu kwa fainali ya kombe la dunia tangu mwaka wa 2002.
Ujerumani Ilifuzu kwa nusu fainali hiyo baada ya kusajili ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ufaransa katika mechi ya robo fainali.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA