ORIGI ASAJILIWA RASMI LIVERPOOL

Divorc Origi katika mojawapo ya mechi za Ubelgiji
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ubelgiji Divorc Origi hatimaye amejiunga na timu ya Liverpool.
Baba yake Origi, Mike Okoth, ambaye ni mchezaji wa zamani wa timu taifa ya Kenya Harambee Stars amethibitsha mwanawe Divorc amesaini mkataba na Liverpool ambao walifurahishwa na mchezo wake mzuri alipoiwakilisha Ubelgiji kwenye kombe la dunia.


Wakati huo huo BEKI wa kimataifa wa Croatia, Dejan Lovren amekamilisha uhamisho wake kutua Liverpool kwa dau la Pauni 20 kutoka Southampton.

Sasa mchezaji huyo anaweka rekodi ya kuwa beki ghali zaidi kuwahi kusajiliwa na Wekundu hao wa Anfield akipiku dau la Pauni Milioni 18.6, ambalo Liverpool ililipa kumsajili beki wa Paris St Germain, Mamadou Sakho Septemba mwaka jana.

Lovren, ambaye amekuwa mlengwa chaguo la kwanza la beki wa kati katika mawindo ya kocha Brendan Rodgers dirisha hili la usajili, amesaini mkataba wa miaka minne baada ya kufuzu vipimo vya afya Merseyside.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA