GERRARD ASTAAFU SOKA LA KIMATAIFA
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Nahodha wa timu ya taifa ya England Steven Gerrard, 34, amestaafu kucheza soka la kimataifa baada ya kuitumikia nchi yake katika kombe la dunia iliyomalizika hivi karibuni nchini Brazil na kuondoshwa katika hatua za awali.
Akizungumza kwenye tovuti ya chama cha soka cha England FA amesema: "nimefurahia kila dakika niliyowakilisha nchi yangu na ni siku ya masikitiko kufahamu sitovaa tena jezi ya England."
Gerrard ameichezea England kwa miaka 14. Anastaafu katika timu ya taifa akiwa hajapata mafanikio yoyote hivyo anawapisha wengine waweze kujaribu kuiletea heshima nchi yake.
Gerrard sasa anasalia na kitambaa cha unahodha katika klabu chake cha Liverpool ambapo katika msimu uliopita wameshindwa kubeba ndoo la ligi ya premia licha ya kuongoza ligi hadi sekunde za mwisho na kupokwa uongozi na Man City.
Gerrard anastaafu wakati timu yake ya England ikishindwa katika hatua za mwanzo katika michuano ya kombe la dunia iliyofanyika nchini Brazil ambapo Ujerumani ilitawazwa mabingwa kwa kuibanjua Argentina 1-0.
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine