MBWANA SAMATTA ATUMA SALAMU ZA POLE KWA BRAZIL
Straika wa kimataifa Mbwana Samata wa Tanzania, amesema atatua nchini Julai 16 (Jumatano ijayo) ili kuongeza nguvu katika kikosi cha Taifa Stars kinachojiandaa kuikabili Msumbiji kuwani tiketi ya kushiriki fainali zijazo za Mataifa ya Afrika (AFCON).
Samata ambaye alikuwa na majeraha yaliyomfanya akose mechi ya marudiano ya Taifa Stars dhidi ya Zimbabwe mwezi uliopita, amesema kwa sasa yupo fiti japo hajacheza mechi yoyote tangu apone.
“Nitakuja kambini tarehe 16, inshallah panapo majaliwa, ninaendelea vizuri kwa sasa japokuwa sijacheza mchezo wowote tangu nilipotoka katika maumivu,” alikaririwa Samata jana na moja ya mitandao ya michezo nchini.
Samata, mshambuliaji wa mabingwa mara nne wa Afrika, Klabu ya TP Mazembe ya DR Congo, ni mmoja kati ya wachezaji muhimu wa Taifa Stars katika kipindi cha miaka mitatu sasa na atatua nchini kuungana na kikosi hicho cha kocha Martin Nooij kilichoweka kambi mjini Tukuyu, Mbeya.
Stars itacheza dhidi ya Msumbiji Jumapili Julai 20, mwaka huu katika mechi ya kwanza ya hatua ya pili ya mtoano ili kuingia katika hatua ya makundi ya fainali hizo zitakazofanyika Morocco mwakani.
KIPIGO BRAZIL
Aidha, Samata amesema kipigo cha mabao 7-1 ambacho timu ya taifa ya Brazil imekipata kutoka kwa Ujerumani ni aibu lakini matokeo hayo yachukuliwe kuwa sehemu ya mpira wa miguu.
Ujerumani iliwapiga bila huruma wenyeji hao wa Fainali za Kombe la Dunia mwaka huu katika mechi ya nusu fainali usiku wa kuamikia juzi.
"Hakika Brazil wamepata aibu kubwa ukizingatia ni wenyeji, ila ndiyo mpira ulivyo," alisema Samata.
Wakati huo huo, viungo Jonas Mkude (Simba) na Himid Mao (Azam) wameanza mazoezi na Taifa Stars huko Tukuyu, Mbeya baada ya kupona majeraha yaliyokuwa yakiwasumbua.
Daktari wa timu hiyo, Billy Haonga jana alilithibitishia NIPASHE kupona kwa wachezaji hao na kuanza kufanya mazoezi, Mkude alikuwa akisumbuliwa na majeraha ya goti wakati Mao alikuwa na maumivu ya nyama za paja.