LIVERPOOL YAMSAJILI MARKOVIC KWA PAUNI MIL 20
Pauni millioni 20 ndicho kima imekitumia Liverpool kumhamisha Lazar Markovic kutoka Benfica.
Mserbia huyo aliiwezesha Benfica kutwaa taji la
Ureno msimu uliopita na anasema anamatumaini makubwa ya kuwaridhisha
mashabiki na mwenye club hiyo.Hata hivyo hilo halijashukisha dau la Suarez sanaa kwani Liverpool waatavuna £75m kutoka Barcelona ambako Suarez sasa amepata makao mapya.
Hivyo ili kujiimarisha kwa kampeni yao ya msimu unaokuja wa Champions League na Premier League walioambulia nafasi ya pili kinyume na matarajio ya wengi, Markovich mwenye umri wa miaka 20 anakuwa mchezaji wa nne kupata mkataba na Liverpool hivi karibuni.
Kumbuka Liverpool pia inasubiri uamuzi wa Divock Origi, mwenye asili ya Kenya , aliyatamba kweli katika safu ya ushambuliaji akiwa kombe la dunia na timu yake ya Ubeleji.
Kweye umri wa miaka 19 pekee wengi wanasubiri kwa hamu kuona Je Liverpool itatumia pesa ngapi kumpata Origi.