VJ PENNY, WEMA SEPETU WAMALIZA BIFU LAO LILILOTOKANA NA PENZI LA DIAMOND PLATINUMZ

Wema Sepetu na VJ Penny wamemaliza beef lao lililokuwepo kwa muda mrefu sasa baada ya Penny kuingilia uhusiano wa Wema na Diamond.

Hata hivyo Wema ameamua kumsamehe Penny wakati huu wa mwezi  mtukufu wa Ramadhani "Kwa moyo mweupe, nasema nimemsamehe Penny, hata nikikutana naye popote nitasalimiana naye kama kawaida', alisema na kuongeza.

'Nimeamua kuachana na yote, mimi ni binti wa Kiislam na nahitaji sana swaumu yangu ipokelewe vyema kwa Mungu." alisema Wema wakati akizungumza na mwandishi wetu.


Nae Penny alipotafutwa alisema "Siwezi kusema nitamchukia Wema ila nimekubali matokeo, sina tatizo naye tena ingawa najua hatuwezi kuwa marafiki tena  kama zamani, lakini yaliyopita yameshapita.”

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA