Ruka hadi kwenye maudhui makuu

BREKING NEWS ZA USAJILI BARANI ULAYA

Kiungo wa Juventus Arturo Vidal, 27, amewapa matumaini zaidi Manchester United baada ya kukiri kuwa "angependa kuichezea moja ya klabu kubwa duniani" ingawa amesema hatolazimisha uhamisho wake (Independent)

United pia wamepata matumaini baada ya winga wa Real Madrid, Angel Di Maria, 26, kukataa kwenda Paris St- Germain (Daily Mirror), beki wa Atlètico Madrid, Filipe Luis, 28, anajiandaa kufanya vipimo vya afya kabla ya kuhamia Chelsea kwa ada ya pauni milioni 20 (Daily Express)


Boss wa Sevilla Unai Emery amesema anajiandaa kumpoteza beki wake wa kushoto Alberto Moreno, 22, ambaye anasakwa na Liverpool (Talksport), mshambuliaji wa Paris St-Germain Edison Cavani, 27, amemtaka wakala wake kumtafutia timu katika Ligi Kuu ya England (Sky Sports)

Arsenal wapo tayari kuacha kumfuatilia kiungo wa Real Madrid Sami Khedira, 27, kufuatia kudai mshahara mkubwa. Khedira anataka kuwa mchezaji anayelipwa zaidi Emirates (Daily Mirror)

Arsenal wanaongeza ufuatiliaji wa beki wa kulia wa Southampton Calum Chambers, 19, licha ya kuwa wanakaribia kumchukua Mathieu Bebuchy, 28, kutoka Newcastle (Daily Mail), beki wa zamani wa Manchester United Rio Ferdinand, 35, atasaini kuichezea QPR siku ya Jumanne (Sky Sports)

Liverpool huenda wakipanda dau la pauni milioni 44 kumtaka mshambuliaji wa Borussia Dortmund Marco Reus, 25, (Daily Express), Dynamo Moscow wamekubaliana na Marseille kumsajili Mathieu Valbuena, 29, kwa pauni milioni 5.5.

Arsenal, Tottenham na West Ham zilikuwa zikimtaka pia (Talksport), Robin Van Persie amepewa wiki tatu za kupumzika na Manchester United baada ya Kombe la Dunia, huku Wayne Rooney wa England akitakiwa kuripoti kambini mapema (Sun)

Kiungo wa Arsenal Jack Wilshire, 22, aliyeomba radhi mwezi Oktoba kwa kuonekana akivuta sigara, ameonekana tena akifanya hivyo mjini Las Vegas akiwa na Joe Hart (Daily Mail)

Arsenal watataka Chris Smalling kujumuishwa kwenye mkataba wowote iwapo Manchester United watamchukua Thomas Vermaelen (Metro) Newcastle wamekamilisha usajili wa Daryl Janmaat wa pauni milioni 5, kuziba nafasi ya Mathieu Debuchy (Guardian).
 

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetoa orodha ya viwango vya ubora wa klabu barani, Simba ikiendelea kuwa juu ya klabu nyingine za Tanzania, nafasi ya tano. Orodha hiyo imetoka leo kuelekea droo ya hatua za awali za michuano ya klabu Afrika ambayo kwa mara ya kwanza kihistoria itafanyika nchini katika studio za Azam Tv, Tabata Jijini Dar es Salaam. Yanga ambayo kama Simba itashiriki Ligi ya Mabingwa — yenyewe inashika nafasi ya 12, wakati timu nyingine katika orodha hiyo ni Namungo FC wanaoshika nafasi ya mwisho, ya 75 kwa pamoja na Salitas FC ya Burkina Faso, Ahli Benghazi ya Libya na NAPSA Stars ya Zambia. Kwa msimu ujao mbali na Simba na Yanga kushiriki Ligi ya Mabingwa, Azam FC na Singida Black Stars zitashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

Miongoni mwa viungo wa pembeni wanaofanya vizuri ni Benodict Khalfan Ngassa ambaye amekuwa akifanya vizuri. Ngassa ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Pamba Jiji na Simba SC, Khalfan Ngassa, pia ni mdogo wa kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Simba na Azam, Mrisho Ngassa anatajwa ni mmoja kati ya wachezaji wanaotazamiwa kufanya makubwa siku za usoni. Mambo Uwanjani Blog itawaletea Makala maalum ya kiungo huyo hatari ambaye ndoto zake ni kufuata nyayo za kaka yake Mrisho Ngassa. Beno Ngassa

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe