USAJILI ULAYA WAZIDI KUPAMBA MOTO
Southampton wanataka kubaki na kiungo wao Morgan Schneiderlin, 24, na watawaambia Tottenham na Arsenal watahitaji kutoa zaidi ya pauni milioni 27 kama wanamtaka (Guardian)
Boss mpya wa Southampton, Ronald Koeman amekataa pauni milioni 3.25 kutoka Cardiff kumsajili beki Jose Fonte, 30 (Daily Mirror)
Barcelona wanafikiria kumchukua beki wa kati Thomas Vermaelen, 28, kutoka Arsenal, ambaye pia anasakwa na Manchester United (Sun), Arsenal wamepewa nafasi ya kumsajili mshambuliaji wa AC Milan Mario Balotelli, 23, kwa pauni milioni 7.9 pamoja na kubadilishana na winga kutoka Costa Rica, Joel Campbell (Metro)
QPR wanazungumza na Marseille kumchukua kiungo wa Ufaransa Mathieu Valbuena, 29, ingawa Dynamo Moscow pia wanamtaka (Daily Mirror), Everton wana matumaini ya kukamilisha uhamisho wa pauni milioni 18 wa mshambuliaji wa Chelsea, Romelu Lukaku, 21 baada ya kuwasili kwa Didier Drogba, 36, Darajani (Daily Express)
Everton pia wanatazama uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa Monaco Lacina Traore, 23, kwa mkopo (Times), boss wa Roma Rudi Garcia amesema kiungo Kevin Strootman, 24, hana mpango wa kwenda Mancheter United msimu huu (Sky Sports)
Liverpool wametoa dau la pauni milioni 14.2 kumtaka winga wa Bayern Munich Xherdan Shaqiri, 22 (Daily Star), West Ham wamekuwa na mazungumzo na mshambuliaji wa Besitkas Hugo Almeida, 30, baada ya Andy Carroll kuumia (Times)
Atlètico Madrid wanamtaka mshambuliaji wa Real Sociedad, Antoinne Griezmann, ambaye anafuatiliwa na Tottenham pia (Daily Express), mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney, 28, anataka kuwa nahodha wa klabu hiyo na anaamini huenda akalibeba Kombe msimu unaokuja (Manchester Evening Standard)
Kiungo wa Man U Tom Cleverly, 24, ana uhakika atarejea katika 'form' chini ya Louis van Gaal baada ya kuwa na wakati mgumu enzi za David Moyes (ESPN), Wojciech Szcesny, 24, atasalia kuwa kipa namba moja wa Arsenal licha wa kuwasili kwa David Ospina, 25 kutoka Nice (Daily Express)
Chelsea bado wanamfuatilia beki wa Real Madrid Rafael Varane, ambaye yupo katika mazungumzo juu ya mkataba mpya (The Independent), Real Madrid huenda wakamchukua mshambuliaji wa Colombia Radamel Falcao kwa mkopo na mshahara wa euro milioni 12 kwa mwaka (ABC)
Everton wanamfuatilia kwa makini winga wa AIK Nabil Bahoui, 23 (Sky Sports), Edinson Cavani anataka kuondoka Paris Saint-Germain, huku Manchester United wakiwa wanamtazama mchezaji huyo wa Uruguay (Le 10 Sport)
Hatma ya Angel Di Maria inatarajiwa kuamuliwa siku chache zijazo, huku Real Madrid wakiwa tayari kupokea dau la euro milioni 50 hadi 60 kutoka kokote (Cadena Cope)
Liverpool huenda wakamkosa Divock Origi baada ya Atlètico Madrid kumtaka mchezaji huyo wa Ubelgiji, kufuatia kuondoka kwa Diego Costa, Adrian na David Villa (Marca) Arsenal wanakaribia kumsajili beki Calum Chambers kutoka Southampton (Sky Sports)