EVRA AENDA JUVENTUS
Patrice Evra amekamilisha uhamisho wake kutoka Manchester United kwenda Juventus.
Beki huyo wa kushoto kutoka Ufaransa amekaa Old Trafford tangu mwaka 2006. Manchester United ime tweet ikisema: Patrice Evra ameondoka #mufc kujiunga na Juventus.
Kila mmoja katika klabu hii anamshukuru kwa miaka yake mingi ya huduma bora aliyotoa."
Hata hivyo Evra ameondoka Man United baada ya kuona ujio wa Luios Van Gaal na huenda asipate nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza baada ya kuondoka kwa David Moyes na mtangulizi wake Alex Furguson.