STRAIKA WA IVORY COAST AMALIZANA NA SIMBA
Mshambuliaji wa timu ya soka ya Taifa ya Burundi, Pierre Kwizera, ambaye alikuwa nchini akifanya mazungumzo na uongozi wa Simba, ameondoka juzi usiku kurejea Ivory Coast kwa lengo moja la kwenda kuvunja mkataba na klabu yake ya Afad Abdijan.
Mchezaji huyo anayecheza nafasi zaidi ya mbili uwanjani, amewaambia viongozi wa Simba kwamba atahakikisha anamalizana na Afad Abdijan na kurejea jijini Dar es Salaam kuitumikia klabu hiyo katika msimu ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
"Kuna mambo naenda kumalizia huko, ila nitarudi Tanzania kucheza Simba," alisema kwa kifupi mchezaji huyo.
Habari kutoka uongozi wa Simba zinaeleza kuwa mchezaji huyo atarejea jijini Agosti 28, mwaka huu tayari kuanza mazoezi na wachezaji wenzake wa timu hiyo.
Kiongozi huyo alisema kuwa Kwizera, amepanga kumalizana kwa busara na viongozi wake wa klabu hiyo ya Ivory Coast ndipo asaini mkataba mpya na Simba.
"Ila ametuhakikishia anarejea Simba," alisema kiongozi huyo ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji na Kamati ya Usajili.
Simba inajipanga kuimarisha kikosi ili iweze kurejesha heshima yake iliyopoteza msimu uliopita kwa kumaliza ikiwa katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi.
Pia, Simba bado iko katika mipango ya kumnasa kiungo mshambuliaji wa timu ya KCB na timu ya Taifa ya Kenya (Harambee Stars), Paul Kiongera.
Rais wa Simba, Evans Aveva, yupo Nairobi, Kenya kukamilisha mazungumzo na nyota huyo ambaye alishawahi kufanya kazi na Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic, katika timu ya Gor Mahia.
Azam ndio mabingwa wa msimu uliopita huku Yanga ikiwa ya pili na timu iliyoshiriki kwa mara ya kwanza, Mbeya City, ilimaliza ligi ikiwa ya tatu.
Kikosi cha Simba cha msimu ujao kitatambulishwa rasmi katika Tamasha la Simba Day ambalo mwaka huu litafanyika Agosti 9 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.