LIVERPOOL KUWANUNUA ORIGI NA MARKOVIC, SUAREZ ANAKWENDA BARCELONA
Liverpool ya Uingereza
imekubaliana na klabu ya Lille kumsajili mshambulizi wa Ubeljiji ambaye
ni mzaliwa wa Kenya Divock Origi .
Origi hata hivyo anatarajiwa kukamilisha mazungumzo juma lijalo .
Klabu hiyo vilevile inapania kukamilisha makubaliano na Markovic, ambaye ataigharimu takriban pauni milioni £25m.
Barca imeonesha niya ya kumnunua Suarez fauka ya matatizo yaliyokumba baada ya kumngata mlinzi wa Italia Chiellini katika mechi ya kombe la dunia .
Liverpool vilevile inamtaka Alexis Sanchez, katika uhamisho huo wa Suarez .
Emre Can,20, vilevile ameshadunda Anfield.
Kocha Brendan Rodgers anatafuta kuimarisha kikosi chake kabla ya kushiriki mchuano wa kuwania ubingwa wa bara uropa mwakani baada ya kumaliza katika nafasi ya pili msimu uliopitanyuma ya Manchester City.