BALOTELLI AFANYA MATANUZI YA 'SIJALI LOLOTE' MAREKANI
Mshambuliaji huyo wa Milan, ambaye alipigwa faini na klabu yake kwa kuvuta sigara kwenye treni mwaka jana, haonekani kabisa kuwa na dalili za kuacha sigara baada ya kupigwa picha akiwa kwenye korido la hoteli anavuta.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 yupo mapumzikoni na mpenzi wake, Fanny Neguesha baada ya Kombe la Dunia ambako alifunga bao moja tu dhidi ya England, Italia ikitolewa hatua ya makundi.
Mtaliano huyo awali alisema kwamba kama asingekuwa mwanasoka, angeibukia kwenye mchezo wa sanaa za mapigano.
Balotelli anafikiriwa yuko njiani kuondoka Milan, ambako alitua miezi 18 iliyopita akitokea Manchester City.
Milan iko tayari kumuuza mshambuliaji huyo ili kupunguza bajeti yao ya mishahara, huku Arsenal ikiwa miongoni mwa klabu zinazomtaka.
Balotelli anataka kurudi Ligi Kuu ya England, lakini kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amekanusha kuwa na mpango wa kumsaini mshambuliaji huyo.