Ruka hadi kwenye maudhui makuu

SHILOLE ATANGAZA KUWANIA UBUNGE JIMBO LA IGUNGA 2015

Muigizaji wa filamu na mwanamuziki Shilole ametangaza nia yake ya kugombea Ubunge katika Jimbo la Igunga anakotokea katika uchaguzi mkuu ujao 2015.

Shilole ameyasema hayo kupitia kipindi cha Sizi za Kitaa cha Clouds TV huku ile collabo yake na Jennifer Lopez wa Marekani ikiwa bado inasubiriwa na mashabiki wake."Baada ya Dr. Dalali Kafumu anayefuata ni mimi, mimi nadhani napenda jimbo langu na napenda wakazi wangu wa Igunga wananiona toka nakua mpaka sasa hivi, kwahiyo wanafurahi, sasa wananiambia sisi hatutaki kumpa mtu mwingine kiti hiki sasa wananipa changamoto.


Vitu viwili vya kwanza ambavyo nitavifanya nikiingia kwenye lile bunge nikiwa kama msanii kwanza natetea haki za wasanii, cha pili Igunga yangu wapo wakazi vijana wapate kazi, yaani akina mama, wale mama lishe na wengine lazima wawe na kazi zao. kwahiyo nitawatafutia kazi. nitajenga chuo cha muziki" alisema shilole

"Mimi jimbo langu nalijua na nimekulia pale mpaka nimekuwa mkubwa lazima nilitimize sitaki wananchi wangu wapate tabu.

Mimi nadhani wanaoenda kugombea majimbo yasiyo ya kwao wanaweza kufanya chochote lakini kama wewe ni mzaliwa wa hapo itakuuma, lakini unakuta mtu wa Dar es salaam anakwenda kugombea Mtwara huko nani anamjua? mimi nitaenda kugombea kwangu lazima nitapata kura lazima watanipa ! kwa hiyo kaeni tayari Shilole ni mbunge mtarajiwa" alijitapa Shilole.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetoa orodha ya viwango vya ubora wa klabu barani, Simba ikiendelea kuwa juu ya klabu nyingine za Tanzania, nafasi ya tano. Orodha hiyo imetoka leo kuelekea droo ya hatua za awali za michuano ya klabu Afrika ambayo kwa mara ya kwanza kihistoria itafanyika nchini katika studio za Azam Tv, Tabata Jijini Dar es Salaam. Yanga ambayo kama Simba itashiriki Ligi ya Mabingwa — yenyewe inashika nafasi ya 12, wakati timu nyingine katika orodha hiyo ni Namungo FC wanaoshika nafasi ya mwisho, ya 75 kwa pamoja na Salitas FC ya Burkina Faso, Ahli Benghazi ya Libya na NAPSA Stars ya Zambia. Kwa msimu ujao mbali na Simba na Yanga kushiriki Ligi ya Mabingwa, Azam FC na Singida Black Stars zitashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

Miongoni mwa viungo wa pembeni wanaofanya vizuri ni Benodict Khalfan Ngassa ambaye amekuwa akifanya vizuri. Ngassa ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Pamba Jiji na Simba SC, Khalfan Ngassa, pia ni mdogo wa kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Simba na Azam, Mrisho Ngassa anatajwa ni mmoja kati ya wachezaji wanaotazamiwa kufanya makubwa siku za usoni. Mambo Uwanjani Blog itawaletea Makala maalum ya kiungo huyo hatari ambaye ndoto zake ni kufuata nyayo za kaka yake Mrisho Ngassa. Beno Ngassa

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe