Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Septemba, 2025

Tatu Malogo, Amina Kyando waula CAF

Waamuzi wa Tanzania Tatu Malogo, Zawadi Yusuph, Glory Tesha, na Amina Kyando wameteuliwa na CAF kuchezesha mchezo wa Kufuzu Kombe la Dunia Wanawake Namibia vs Zambia utakaochezwa Dobsonville, Johannesburg, Afrika Kusini Oktoba 22, 2025. 

Yanga yaibana Mbeya City Sokoine

Ni ngumu kuamini lakini ndivyo ilivyotokea, mabingwa watetezi wa Ligi Kuu bara Yanga SC jioni ya leo imeilazimisha Mbeya City kwenda nayo sare tasa 0-0 uwanja wa Sokoine mjini Mbeya. Ingawa Yanga ndio imeibana Mbeya City kwakuwa ilikuwa ugenini, lakini mashabiki wake wameyapokea vibaya matokeo hayo kwani timu yao itakuwa na pointi 4 na ikiachwa nyuma na wapinzani wake Azam FC na Singida Black Stars wenye pointi 6 na Simba kama kesho itaibuka na ushindi.

Singida Black Stars ya Gamondi mwendo mdundo Ligi Kuu bara

BAO pekee la mshambuliaji Mkenya, Elvis Baranga Rupia dakika ya 45’+5 limeipa Singida Black Stars ushindi wa 1-0 dhidi ya Mashujaa FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam. Black Stars wanafikisha pointi sita katika mchezo wa pili, wakati Mashujaa inabaki na pointi zake nne baada ya kucheza mechi tatu sasa ikishinda moja, sare moja na kufungwa moja leo.

Nasreddine Nabi kutambulishwa Simba

Taarifa zilizonifikia punde ni kwamba kocha wa zamani wa mabingwa wa soka nchini Yanga SC na Kaizer Chief ya Afrika Kusini, Nasreddine Nabi anatambulishwa na Simba SC. Baada ya mabingwa hao wa zamani nchini kuachana na kocha wake Fadlu David's raia wa Afrika Kusini, imegeukia kwa Nabi ambaye ameachana na Kaizer Chief. Lakini zipp taarifa nyingine kwamba Nabi amewasili nchini kwa ajili ya kurejea kwenye klabu yake ya zamani ya Yanga ambayo kocha wake Roman Folz aendani nao.

Kocha aliyeitosa Yanga afikiria kuondoka ASEC Mimosas

Msimu uliopita ndio mkataba wangu na Asec Mimosas ulifika ukingoni, mabosi waliniita mezani tukazungumza na tukafikia uamuzi wa kuongeza kandarasi. Siwezi zungumzia sana hatima yangu ndani ya Asec kwasasa kisa mchezo mmoja na ikitokea hivyo maamuzi yote yatafanywa na management yangu ila kiufupi huu ndio wakati sahihi wa kuanza kuwaza kuhusu hilo" "Majuto ni makubwa kwasababu tulitakiwa kumaliza huu mchezo ugenini siku yakwanza lakini tumeshindwa kufanya hivyo na leo tumetolewa CAFCL katika hatua za mwanzo kabisa.. Kama nitaendelea kusalia Asec naamini bado nina mambo mengi makubwa ya kufanya ana moja yapo ni kuhakikisha tunatwaa makombe yote ya ndani kwa msimu huu." Ikumbukwe kocha huyu alikuwa akihusishwa kujiunga na Yanga kama kocha mkuu huku Roman Folz akiwa msaidizi na baadaye akaitosa Yanga na kusalia ASEC jambo ambalo liliwachanganya mabosi wa Yanga, sasa anafikiria kuondoka 

Heri Mzozo aliomba laki 6 akapewa milioni 15 na Tshabalala

Meneja wa mchezaji wa Yanga SC Mohamed Hussein Zimbwe anayejulikana kwa jina la Carlos Mastermind amejibu malalamiko ya mlezi wa kisoka wa Mohamed Hussen anayejulikana  kwa jina la Heri Mzozo (Kheri Chibakasa). Carlos amejibu baada ya awali Heri Mzozo kusikika katika vyombo vya habari akidai kuwa amewasaidia wachezaji wengi ila hakuna anayemjali baada ya kufanikiwa na wanaishi maisha mazuri ilihali yeye kapanga ameshindwa hadi kumalizia nyumba yake. Carlos akihojiwa na Clouds alisema kuwa Mohamed Hussein amewahi kumpa Heri Mzozo milioni 15 amalizie nyumba yake baada ya awali kupiga simu kuomba laki sita za Kodi. “Samahani kama nitakuwa namdhalilisha ila hii lazima niweke wazi kama shuhuda, mwaka juzi Heri alinipigia akaniambia mimi nadaiwa kodi laki sita, kesho yake nikampigia yeye pamoja na Tshabalala (Mohamed Hussein) ishu ikiwa kwa nini hadi sasa hivi ana shida ya kodi ya nyumba” “Tukafika tukaongea na nikasema suluhu hapa sio kodi,leo Tshabalala anaitoa hii laki sita baada ya m...

Afrika Kusini yaadhibiwa na FIFA kwa udanganyifu

Kamati ya Nidhamu ya FIFA imekiadhibu Chama cha Soka cha Afrika Kusini (SAFA) kwa kumchezesha mchezaji asiye halali, Teboho Mokoena, katika mchezo wa Afrika Kusini dhidi ya Lesotho uliochezwa tarehe 21 Machi 2025 kwenye mashindano ya awali ya Kombe la Dunia la FIFA 2026™, hivyo kukiuka kifungu cha 19 cha Kanuni za Nidhamu za FIFA (FDC) na kifungu cha 14 cha Kanuni za Mashindano ya Awali ya Kombe la Dunia la FIFA 2026™. Hivyo basi, Kamati ya Nidhamu ya FIFA imetangaza kuwa mchezo husika umetwaliwa (umepotezwa kwa makosa) na timu ya taifa ya Afrika Kusini kwa matokeo ya 3-0. SAFA pia imeamriwa kulipa faini ya CHF 10,000 kwa FIFA, huku Teboho Mokoena akipewa onyo. Pande husika zilijulishwa kuhusu uamuzi wa Kamati ya Nidhamu ya FIFA leo. Kwa mujibu wa masharti husika ya FDC, wana siku kumi kuomba uamuzi wenye maelezo ya kina, ambao, iwapo ukiombwa, utachapishwa baadaye kwenye legal.fifa.com. Uamuzi wa kutwaliwa kwa mchezo bado uko chini ya haki ya kukata rufaa mbele ya Kamati ya Rufaa ya F...

Simba SC yawashukuru Morocco na TFF

Shukrani za dhati kwa Kocha Hemed Suleiman ‘Morocco’ kwa kuongoza kikosi chetu katika mchezo muhimu wa jana wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Gaborone United, na kufanikiwa kutuvusha. Shukrani pia kwa Shirikisho la Soka nchini (TFF) kwa kumruhusu Kocha Morocco ambaye ni Kocha wa Taifa Stars kujiunga nasi. 

Hamad Ally kumrithi Fadlu Simba SC

Baada ya kufuzu raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika chini ya kaimu kocha mkuu Hemed Suleiman 'Morocco', uongozi wa Simba SC umetuma maombi ya kumhitaji kocha wa JKT Tanzania, Hamad Ally, ili ajiunge kama kocha msaidizi. Hii inakuja wakati Simba ikiwa katika harakati za kumtafuta kocha mkuu mpya, kufuatia makubaliano ya kuachana na aliyekuwa kocha wao, Fadlu Davids. Kwa sasa, Morocco amepewa jukumu la kukaimu nafasi hiyo. Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika kilichoeleza Mwanaspoti, Simba tayari imefanya mazungumzo na Hamad Ally ili awe sehemu ya benchi la ufundi akisaidiana na Morocco pamoja na Seleman Matola.

Mbeya City waapa kuifunga Yanga kesho

Kuelekea mchezo wa kesho kati ya wenyeji Mbeya City dhidi ya Yanga SC kocha mkuu wa the purple nation Malale Hamsini amesema kuwa wamejipanga vizuri kuikabili Yanga na kesho wataweka washambuliaji wengi ili kupata ushindi wa alama tatu. Mechi itapigwa kuanzia majira ya 10:15 jioni kwenye dimba la Sokoine jijini Mbeya 

Morocco out Simba

Mkataba kati ya kocha wa muda wa Simba SC, Hemed Suleiman Ali Morocco na klabu ya Simba SC imefikia kikomo hivyo kuanzja sasa kocha huyo hatokuwa ndani ya kikosi hicho. Makubaliano yao ilikuwa asimame kwenye mechi moja tu baada ya kocha msaidizi wa Simba, Seleman Matola kuoneshwa kadi nyekundu kule Botswana hivyo Simba ilimuomba Morocco ambaye ni kocha mkuu wa timu ya taifa, Taifa Stars kukaa benchi kwenye mechi moja dhidi ya Gaborone United. Shukrani kwa Morocco baada ya Simba kufuzu raundi ya kwanza baada ya sare ya 1-1 ikiwa na ushindi wa jumla ya mabao 2-1 baada ya ushindi wa bao 1-0 mjini Gaborone wakati timu ikiwa na Fadlu David's aliyetimkia Raja Casablanca. Sasa timu inarejea mikononi mwa Matola mpaka pale Simba itakapomkabidhi kocha mpya hivi karibuni, Jose Ribeiro kocha wa zamani wa Orlando Pirates na Al Ahly anatajwa kumrithi Fadlu huku pia Mm Miguel Gamondi wa Singida Black Stars naye akitajwa kuchukua nafasi hiyo, ngoja tusubiri na tuone

ASEC Mimosas yatupwa nje CAF

Klabu ya Asec Mimosas ya Ivory Coast imesukumizwa nje ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kufuatia kipigo cha penalti 5-4 baada ya sare ya jumla 1-1 dhidi ya Power Dynamos ya Zambia kwenye hatua ya awali. Power Dynamos itachuana na vigogo wa Uganda, Vipers Sc kwenye raundi ya pili ambapo miamba hiyo ya Zambia itaanzia ugenini, Kitende, Uganda kati ya Oktoba 17-19, 2025 na kurudiana kati ya nyumbani Zambia kati ya Oktoba 24-26, 2025.

Roman Folz akalia kuti kavu Yanga

Huenda mchezo wa Yanga dhidi ya Mbeya city ukawa mchezo wa mwisho kwa kocha  Romain Folz baada ya viongozi wakubwa wa juu wa Yanga kutoridhishwa na mwenendo wa timu  Licha ya Yanga kupata ushindi kwenye mechi zao zote lakini timu hiyo imeonekana kutocheza soka safi  Yanga wameona wamlete kocha mwingine kabla ya kwenda kwenye International Break ili angalau kocha mpya apate muda wa kukaa na timu

Samia aahidi kujenga uwanja wa soka Msoga kimshukuru Kikwete

Mgombea wa urais CCM Dk. Samia Suluhu Hassan ameahidi kuwa katika kipindi cha miaka mitano ijayo ikiwa wananchi watampa ridhaa ya kuunda serikali, kutajengwa uwanja mkubwa wa michezo Msoga, Chalinze Mkoani Pwani. "Hii ni kama shukrani yetu kwa utumishi wa Rais wa awamu ya nne Dk. Jakaya Kikwete, mengi tumeyapa majina Kikwete lakini sio Msoga, hapa hatukufanya kitu kwahiyo uwanja ule tutauweka Msoga kuonesha shukrani yetu kwa Rais wa awamu ya nne," amesema Dk. Samia. Dk. Samia ameyaeleza hayo leo Jumapili Septemba 28, 2025 wakati wa kampeni zake kwenye eneo la Msoga mkoani humo akiwa njiani kuelekea Mkoani Tanga. Pia ameahidi kuendelea kusogeza huduma za kijamii karibu zaidi na wananchi pamoja na kuendelea na uhakiki wa madai ya fidia kwa baadhi ya wananchi wa Msata waliopisha miradi ya maendeleo kwenye eneo hilo.

Conte atemwa Guinea, Camara aitwa

Golikipa wa Klabu ya Simba, Moussa Camara, ameitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Guinea kwa ajili ya michezo ijayo ya kimataifa chini ya kocha Paulo Duarte. Hata hivyo, kiungo wa Klabu ya Yanga, Moussa Balla Conte, hakujumuishwa kwenye kikosi hicho baada ya kocha huyo kutompa nafasi katika orodha ya wachezaji waliotajwa. Guinea ipo mbioni kujiandaa na michezo ya kufuzu Kombe la Dunia/AFCON, na ujio wa Camara unaongeza chachu kubwa ya ushindani kwenye nafasi ya mlinda mlango. 👀 Una maoni gani juu ya maamuzi ya kocha Duarte kumuita Camara na kumwacha Balla Conte nje ya kikosi?

Coastal Union yamtimua kocha wake

Wana Mangushi, Coastal Union ya Tanga imeamua kumpa virago kocha wake Ally Mohamed Ameir baada ya kupoteza mechi mbili mfululizo za Ligi Kuu bara na kitishia mwenendo wake msimu huu. Kocha huyo ameiongoza Coastal Union kwenye michezo (3) ya Ligi pekee huku akifanikiwa kushinda mchezo (1) pekee na kupoteza michezo (2). MATOKEO YA MICHEZO (3) YA COASTAL UNION Coastal Union 1-0 Tanzania Prisons Coastal Union 1-2 JKT Tanzania Dodoma Jiji 2-0 Coastal Union Tayari maamuzi ya kumfungashia virago Kocha Ameir yamefanyika na kinachosubiriwa ni Taarifa kwa Umma ambayo itatolewa hapo kesho.

Simba yavuka kwa mbinde Ligi ya mabingwa

TIMU ya Simba SC imefanikiwa kuingia Hatua ya 32 Bora  Ligi ya Mabingwa Afrika licha ya sare ya kufungana bao 1-1 na Gaborone United ya Botswana katika mchezo wa marudiano wa Raundi ya Kwanza leo Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Mabao yote yalipatikana kwa mikwaju ya penalti, Simba SC wakitangulia kupitia kwa kiungo mshambuliaji Muivory Coast, Jean Charles Ahoua dakika ya 45, kabla ya kiungo mwingine mshambuliaji wa Kimataifa wa Botswana, f Lebogang Ditsele kuisawazishia Gaborone United dakika ya 58. Kwa matokeo hayo, Simba SC inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 2-1 kufuatia ushindi wa 1-0 kwenye mchezo wa kwanza wiki iliyopita Uwanja wa Obed Itani Chilume, zamani Francistown Sports Complex mjini Francistown, Botswana – bao la winga wa Mkongo, Elie Mpanzu Kibisawala dakika ya 16. Simba SC sasa itakutana na Nsingizini Hotspurs ya Eswatini ambayo imeitoa Simba Bhora ya Zimbabwe kwa penalti 4-2 baada ya sare ya jumla ya 1-1 kila timu ikishinda 1-0 mchezo mmoja. ...

Azam FC yachanja mbuga kombe la Shirikisho

TIMU ya Azam FC imefanikiwa kwenda Hatua ya 32 Bora Kombe la Shirikisho Afrika baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Al Merreikh Bentiu ya Sudan Kusini katika mchezo wa marudiano Raundi ya Kwanza Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam. Mabao ya Azam FC yamefungwa na beki wa Kimataifa wa Mali, Yoro Mamadou Diaby dakika ya 18 na kiungo mshambuliaji, Nassor Saadun Hamoud dakika ya 90’+2. Kwa matokeo hayo, Azam FC inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 4-0 kufuatia kuichapa Al Merreikh Bentiu 2-0 pia kwenye mchezo wa kwanza wiki iliyopita Uwanja wa Juba Jijini Juba, Sudan Kusini. Kwenye mchezo huo, mabao ya Azam FC yalifungwa na kiungo wa Kimataifa wa Tanzania, Feisal Salum Abdallah dakika ya 23 na mshambuliaji mpya Mkongo, Bola Jephte Kitambala dakika ya 70. Azam FC saaa itakutana na KMKM ya Zanzibar ambayo imeitoa AS Port ya Djibouti kwa jumla ya mabao 4-2 ikishinda 2-1 kila mechi zote zikipigwa Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.

Gamondi huyoo kuelekea Simba, kesho kuzungumza na Waandishi wa habari

Kocha Mkuu wa Singida Black Stars Miguel Gamondi atazungumza na Vyombo vya Habari kesho Jumatatu kuanzia saa 4:00 asubuhi, katika Makao Makuu ya NBC Bank – Posta, jijini Dar es Salaam. Moja kati ya mazungumzo yake ni kuhusu mpango wake wa kutaka kujiunga na Simba kama imavyosemekana. Waandishi wote wa Habari za Michezo mnakaribishwa.

Yanga yakabidhiwa milioni 10 za mama Samia

Katibu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa amekabidhi Sh. Milioni 10 kwa klabu Yanga, zawadi kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan baada ya ushindi wa 2-0 leo dhidi ya Wiliete SC ya Angola katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Singida Black Stars yahamia uwanja wa KMC

Kutokana na ratiba ilivyobana, mchezo wetu wa nyumbani dhidi ya Mashujaa FC utafanyika Septemba 30 jijini Dar es Salaam, kwenye Uwanja wa KMC saa 10:00 jioni. Uamuzi huu umefikiwa ili kuwapa wachezaji muda wa kupumzika na kujiandaa vyema, hasa baada ya mchezo mgumu wa jana wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Rayon Sports. Baada ya mchezo huo, tutakuwa tumemaliza rasmi ratiba ya mwezi Septemba na timu itarejea nyumbani Singida kwa maandalizi ya michezo ijayo, amesema Hussein Masanza msemaji wa Singida Black Stars 

Singida Black Stars ya Gamondi yatoa dozi

Timu ya Singida Black Stars wanaandika historia ya kuvuka na kwenda hatua inayofuata ya mtoano katika kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya ushindi wa mabao 2-1. Wametinga hatua hiyo baada ya kuwatoa Rayon Sports kutoka Rwanda kwa Aggregate ya 3-1. Mabao ya Singida Black Stars yamefungwa na Idriss Diomande dakika ya 38 na Antony TRA Bi Tra dakika ya 56 wakati bao pekee la Rayon Sports limefungwa na Gloire dakika ya 44.

Rais Samia amzawadia nyumba Alphonce Simbu

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amemzawadia nyumba Mwanariadha wa mbio ndefu, Alphonce Felix Simbu Jijini Dodoma kufuatia Sajinitaji huyo wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kushinda Medali ya Dhahabu kwenye Mashindano ya Dunia wiki mbili zilizopita. Hayo yamelezwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa katika hafla ya kumpongeza mwanariadha huyo leo Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam baada ya kushinda ubingwa wa Dunia wa Marathon Jijini Tokyo nchini Japan Septemba 15. Pamoja na zawadi ya nyumba, Waziri Mkuu, Majaliwa amemkabidhi Simbu hundi yenye thamani ya Shilingi Milioni 20 ambayo ni zawadi kutoka Baraza la Michezo la Taifa (BMT). Awali, akizungumza kwenye hafla hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dk. Samia ina mchango kubwa katika sekta ya michezo. Amesema hivi sasa wamejipanga kuhakikisha Tanzania inashinda tena Medali kweny...

Mlandege yapata ushindi, ila yatupwa nje

Klabu ya Mlandege FC ya Zanzibar wameshinda bao 3-2 kwenye mchezo wa leo dhidi ya Ethiopian Insuarance lakini matokeo ya jumla (3-4) yamewapa nafasi Ethiopian Insuarance ya kusonga mbele kwenye hatua inayofuata ya michuano ya Ligi ya mabingwa Afrika.

Yanga ya pira gimbi, yaifumua Willete 2-0 na kutinga raundi ya kwanza Ligi ya mabingwa Afrika

MABINGWA wa Tanzania, Yanga wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Wiliete SC ya Angola katika mchezo wa marudiano Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Mabao ya Yanga SC katika mchezo huo yamefungwa na viungo, Muivory Coast, Peodoh Pacome Zouzoua dakika ya 70 na mzawa, Aziz Andambwile Mwambalaswa dakika ya 86. Kwa ushindi huo, Yanga inaitupa nje timu hiyo ya Benguela kwa jumla ya mabao 5-0 kufuatia ushindi wa ugenini wa mabao 3-0 dhidi ya Wiliete katika mchezo wa kwanza Uwanja wa Novemba 11, Jijini Luanda nchini Angola, mabao ya Andambwile dakika ya 31, kiungo mwingine Edmund Godfrey John dakika ya 71 na mshambuliaji Mzimbabwe, Prince Dube Mpumelelo dakika ya 79. Sasa Yanga itakutana na Silver Strikers ya Malawi ambayo imeitoa ASSM Elgeco Plus ya Madagascar kwa mabao ya ugenini leo ikitoa sare ya 0-0 Uwanja wa Taifa wa Bingu Jijini Lilongwe kufuatia sare ya 1-1 kwenye mchezo wa kwanza ugenini.

Tanzania Prisons yaipiga KMC ya Maximo

WENYEJI, Tanzania Prisons wameibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya KMC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya. Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, mshambuliaji Oscar Mwajanga Mwasanga dakika ya 14 ya mchezo huo, huo ukiwa ushindi wa kwanza kwa Tanzania Prisons baada ya mechi tatu tangu kuanza kwa msimu huu. Mechi mbili za awali Tanzania Prisons ilifungwa 1-0 mfululizo ugenini dhidi ya Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani, Tanga na Namungo FC Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi. Kwa upande wao KMC wanapoteza mechi ya pili kati ya tatu, nyingine wakifungwa pia 1-0 na Singida Black Stars baada ya kushinda 1-0 na wao katika mchezo wa kwanza dhidi ya Dodoma Jiji mechi zote wakicheza nyumbani Uwanja wa KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam. 

Ibenge aishitukia ligi ya bongo

BAADA ya kucheza na Mbeya City kwenye mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu Bara Tanzania akiwa na Azam FC; Kocha Florent Ibenge amefunguka kuwa ameshaona Ligi ya Bongo ni moja ya Ligi ngumu zaidi barani Afrika. "Si rahisi. Michezo si rahisi, nadhani michuano hii (NBCPL) ni moja ya michuano migumu zaidi barani Afrika. Kwahio tunapaswa kuchukua alama kwa kila mchezo." Alisema Ibenge. Akiongeza kuwa changamoto alizoziona zinamfanya atafute mbinu zaidi za kuliboresha kundi lake kwani hajaridhika na kiwango cha wachezaji.

Arajiga na wenzake kuchezesha kombe la Dunia

Waamuzi wa Tanzania Ahmed Arajiga, Mohamed Mkono, Said Hamdan na Nasir Salum wameteuliwa na FIFA kuchezesha mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia Cape Verde vs Eswatini utakaochezwa katika uwanja wa Taifa, Praia Octoba 13, 2025.

Sheria Ngowi avunja mkataba na Gor Mahia

Klabu ya Gor Mahia ya nchini Kenya imevunja rasmi mkataba na mbunifu wa jezi zao ndg Sheria Ngowi ambaye ndiye alitengeneza jezi za klabu hiyo msimu uliopita. Huo ni mkataba wa pili kuuvunja, hasa baada ya kuanza kuvunja mkataba na klabu ya Yanga SC ya Tanzania.

Jose Ribeiro kocha mkuu Simba

Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Al Ahly ya Misri na Orlando Pirates ,ya Afrika Kusini José Ribeiro ndiye mgombea anayeongoza kuwa Kocha Mpya wa Simba SC  Simu zinaita simba wanahitaji huduma yake mpka sasa mazungumzo yanaendelea na tajiri Simba ni timu kubwa makocha wengi kutoka Nchi mbali mbali wanahitaji kufanya kazi na Simba.

Yanga itakaa sawa chini yangu - Folz

Kocha mkuu wa Yanga SC, Roman Folz raia wa Ufaransa, amesema kikosi chake kitakaa sawa hivi karibuni na amewataka mashabiki wa timu hiyo kukaa mkao wa furaha. “Kila mchezaji anaeonesha mazoezini atapewa mechi,lakini kila mchezaji atacheza kwenye timu yangu,yote ni kwasababu nawahitaji wawe Fiti muda wote kwasababu mbele kuna mashindano mengi Kwasasa hatuwezi kuwa na huo ubora lakini kuna kipindi kinakuja timu itakuwa bora sana chini yangu” Kocha mkuu wa kikosi cha Yanga Sc”Romain Folz”

Yanga yatambulisha jezi mpya za kimataifa

Mabingwa wa Tanzania bara Yanga SC hii Leo wameachia toleo la pili la jezi mpya ambayo inatambulisha Mdhamini mkuu wa mechi za kimataifa NIA. Kwa upande wa jezi za nyumbani ndio hizo pichani ambapo tofauti ni mbili tu na zile za awali, mzalishaji mpya wa jezi pamoja na kitambaa ambacho ni tofauti na kile cha kwanza.

KMKM yatinga raundi ya kwanza kombe la Shirikisho

TIMU ya KMKM imefanikiwa kuingia Hatua ya Timu 32 ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya AS Port ya Djibouti leo katika mchezo wa marudiano wa Raundi ya Kwanza ya leo Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar. Kwa matokeo hayo, KMKM inakwenda Raundi ya Pili kwa ushindi wa jumla wa 4-2 kufuatia ushindi mwingine wa 2-1 kwenye mchezo wa kwanza wiki iliyopita hapo hapo New Amaan Complex. Sasa KMKM itakutana na mshindi wa jumla kati ya Azam FC na Al Merreikh FC Benteu, maarufu kama Al Merreikh Juba ya Sudan Kusini. Azam FC ipo kwenye nafasi nzuri ya kusonga mbele baada ya ushindi wa 2-0 kwenye mchezo wa kwanza na Al Merreikh FC Benteu mjini Juba nchini Sudan Kusini na timu hizo zitarudiana Jumapili Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

KCMC na KWSC kujenga viwanja vinne vya soka vya kimataifa

Hospital ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini KCMC kwa kushirikiana na Kilimanjaro Wonders Sports Center  mapema leo wamesaini makubaliano ya kujenga Viwanja vinne vya kisasa vya mpira wa miguu vyenye viwango vinavyotambulika na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA). Upande wa KCMC makubaliano hayo yamewakilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Prof. Gileard Masange na kwa upande wa Kilimanjaro Wonders Sports Center ikiwakilishwa na Mkurugenzi Mtendaji Laurent Kinabo.  Lengo kuu la mradi huo ni kuandaa mazingira rafiki ya michezo kwa watoto wenye ulemavu wa ngozi, Watumishi wa KCMC, Wanafunzi , ndugu wa wagonjwa na jamii kwa ujumla. Ujenzi wa Viwanja hivyo unatarajiwa kuanza mapema mwezi Oktoba  Mwaka huu.

Yusuf Kagoma kuikosa Gaborone United Jpili

Yusuf Kagoma (29) atakosa mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika  dhidi ya Gaborone United baada ya kuumia mguu wa kulia. Kagoma aliumia kipindi cha kwanza cha mchezo wa jana dhidi ya Fountain Gates, akaendelea kucheza kwa muda lakini alilazimika kutolewa mapema kipindi cha pili. Uchunguzi umeonyesha jeraha lake ni kubwa kuliko ilivyodhaniwa awali, hivyo hatakuwa sehemu ya kikosi cha marudiano. Simba SC itamkosa mchezaji muhimu katika mchezo huu wa kuamua hatma yao kwenye ligi ya mabingwa.

Simba kukutana na Gaborone United bila mashabiki wake

Rasmi Afisa habari wa Simba SC  Ahmed Ally  amethibitisha  mechi ya Simba SC dhidi ya Gaborone United Jumapili hii haitakuwa na mashabiki wana tumikia adhabu ya CAF. Adhabu hiyo ilitokana na mchezo dhidi ya Al Masry ambapo kuna shabiki aliingia uwanjani na kuna mashabiki waliwasha moto. Adhabu hiyo inakwenda pamoja na faini ya Dola 50,000 Sawa na Tsh  Million 123,