Ni ngumu kuamini lakini ndivyo ilivyotokea, mabingwa watetezi wa Ligi Kuu bara Yanga SC jioni ya leo imeilazimisha Mbeya City kwenda nayo sare tasa 0-0 uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Ingawa Yanga ndio imeibana Mbeya City kwakuwa ilikuwa ugenini, lakini mashabiki wake wameyapokea vibaya matokeo hayo kwani timu yao itakuwa na pointi 4 na ikiachwa nyuma na wapinzani wake Azam FC na Singida Black Stars wenye pointi 6 na Simba kama kesho itaibuka na ushindi.