Wana Mangushi, Coastal Union ya Tanga imeamua kumpa virago kocha wake Ally Mohamed Ameir baada ya kupoteza mechi mbili mfululizo za Ligi Kuu bara na kitishia mwenendo wake msimu huu.
Kocha huyo ameiongoza Coastal Union kwenye michezo (3) ya Ligi pekee huku akifanikiwa kushinda mchezo (1) pekee na kupoteza michezo (2).
MATOKEO YA MICHEZO (3) YA COASTAL UNION
Coastal Union 1-0 Tanzania Prisons
Coastal Union 1-2 JKT Tanzania
Dodoma Jiji 2-0 Coastal Union
Tayari maamuzi ya kumfungashia virago Kocha Ameir yamefanyika na kinachosubiriwa ni Taarifa kwa Umma ambayo itatolewa hapo kesho.