Timu ya Singida Black Stars wanaandika historia ya kuvuka na kwenda hatua inayofuata ya mtoano katika kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya ushindi wa mabao 2-1.
Wametinga hatua hiyo baada ya kuwatoa Rayon Sports kutoka Rwanda kwa Aggregate ya 3-1.
Mabao ya Singida Black Stars yamefungwa na Idriss Diomande dakika ya 38 na Antony TRA Bi Tra dakika ya 56 wakati bao pekee la Rayon Sports limefungwa na Gloire dakika ya 44.