Hospital ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini KCMC kwa kushirikiana na Kilimanjaro Wonders Sports Center mapema leo wamesaini makubaliano ya kujenga Viwanja vinne vya kisasa vya mpira wa miguu vyenye viwango vinavyotambulika na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).
Upande wa KCMC makubaliano hayo yamewakilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Prof. Gileard Masange na kwa upande wa Kilimanjaro Wonders Sports Center ikiwakilishwa na Mkurugenzi Mtendaji Laurent Kinabo.
Lengo kuu la mradi huo ni kuandaa mazingira rafiki ya michezo kwa watoto wenye ulemavu wa ngozi, Watumishi wa KCMC, Wanafunzi , ndugu wa wagonjwa na jamii kwa ujumla.
Ujenzi wa Viwanja hivyo unatarajiwa kuanza mapema mwezi Oktoba Mwaka huu.