Golikipa wa Klabu ya Simba, Moussa Camara, ameitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Guinea kwa ajili ya michezo ijayo ya kimataifa chini ya kocha Paulo Duarte.
Hata hivyo, kiungo wa Klabu ya Yanga, Moussa Balla Conte, hakujumuishwa kwenye kikosi hicho baada ya kocha huyo kutompa nafasi katika orodha ya wachezaji waliotajwa.
Guinea ipo mbioni kujiandaa na michezo ya kufuzu Kombe la Dunia/AFCON, na ujio wa Camara unaongeza chachu kubwa ya ushindani kwenye nafasi ya mlinda mlango.
👀 Una maoni gani juu ya maamuzi ya kocha Duarte kumuita Camara na kumwacha Balla Conte nje ya kikosi?