BAO pekee la mshambuliaji Mkenya, Elvis Baranga Rupia dakika ya 45’+5 limeipa Singida Black Stars ushindi wa 1-0 dhidi ya Mashujaa FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam.
Black Stars wanafikisha pointi sita katika mchezo wa pili, wakati Mashujaa inabaki na pointi zake nne baada ya kucheza mechi tatu sasa ikishinda moja, sare moja na kufungwa moja leo.