Meneja wa mchezaji wa Yanga SC Mohamed Hussein Zimbwe anayejulikana kwa jina la Carlos Mastermind amejibu malalamiko ya mlezi wa kisoka wa Mohamed Hussen anayejulikana kwa jina la Heri Mzozo (Kheri Chibakasa).
Carlos amejibu baada ya awali Heri Mzozo kusikika katika vyombo vya habari akidai kuwa amewasaidia wachezaji wengi ila hakuna anayemjali baada ya kufanikiwa na wanaishi maisha mazuri ilihali yeye kapanga ameshindwa hadi kumalizia nyumba yake.
Carlos akihojiwa na Clouds alisema kuwa Mohamed Hussein amewahi kumpa Heri Mzozo milioni 15 amalizie nyumba yake baada ya awali kupiga simu kuomba laki sita za Kodi.
“Samahani kama nitakuwa namdhalilisha ila hii lazima niweke wazi kama shuhuda, mwaka juzi Heri alinipigia akaniambia mimi nadaiwa kodi laki sita, kesho yake nikampigia yeye pamoja na Tshabalala (Mohamed Hussein) ishu ikiwa kwa nini hadi sasa hivi ana shida ya kodi ya nyumba”
“Tukafika tukaongea na nikasema suluhu hapa sio kodi,leo Tshabalala anaitoa hii laki sita baada ya miezi mitatu itarudi tena, nikamwambia Heri wewe ukipata Tsh ngapi unamaliza nyumba yako?
Akasema akipata milioni 20 anakamilisha kila kitu, nikamwambia Tshabalala hiyo laki sita mpe, halafu hiyo milioni 20 ya kumaliza nyumba yako nitakurudia,.
Baada ya siku saba Tshabalala akampa Heri milioni 15 kati ya 20 aliyohitaji, sasa ameongea kama Tshabalala hajawahi kumsaidia kabisa”