Baada ya kufuzu raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika chini ya kaimu kocha mkuu Hemed Suleiman 'Morocco', uongozi wa Simba SC umetuma maombi ya kumhitaji kocha wa JKT Tanzania, Hamad Ally, ili ajiunge kama kocha msaidizi.
Hii inakuja wakati Simba ikiwa katika harakati za kumtafuta kocha mkuu mpya, kufuatia makubaliano ya kuachana na aliyekuwa kocha wao, Fadlu Davids. Kwa sasa, Morocco amepewa jukumu la kukaimu nafasi hiyo.
Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika kilichoeleza Mwanaspoti, Simba tayari imefanya mazungumzo na Hamad Ally ili awe sehemu ya benchi la ufundi akisaidiana na Morocco pamoja na Seleman Matola.