Mkataba kati ya kocha wa muda wa Simba SC, Hemed Suleiman Ali Morocco na klabu ya Simba SC imefikia kikomo hivyo kuanzja sasa kocha huyo hatokuwa ndani ya kikosi hicho.
Makubaliano yao ilikuwa asimame kwenye mechi moja tu baada ya kocha msaidizi wa Simba, Seleman Matola kuoneshwa kadi nyekundu kule Botswana hivyo Simba ilimuomba Morocco ambaye ni kocha mkuu wa timu ya taifa, Taifa Stars kukaa benchi kwenye mechi moja dhidi ya Gaborone United.
Shukrani kwa Morocco baada ya Simba kufuzu raundi ya kwanza baada ya sare ya 1-1 ikiwa na ushindi wa jumla ya mabao 2-1 baada ya ushindi wa bao 1-0 mjini Gaborone wakati timu ikiwa na Fadlu David's aliyetimkia Raja Casablanca.
Sasa timu inarejea mikononi mwa Matola mpaka pale Simba itakapomkabidhi kocha mpya hivi karibuni, Jose Ribeiro kocha wa zamani wa Orlando Pirates na Al Ahly anatajwa kumrithi Fadlu huku pia Mm Miguel Gamondi wa Singida Black Stars naye akitajwa kuchukua nafasi hiyo, ngoja tusubiri na tuone