Mgombea wa urais CCM Dk. Samia Suluhu Hassan ameahidi kuwa katika kipindi cha miaka mitano ijayo ikiwa wananchi watampa ridhaa ya kuunda serikali, kutajengwa uwanja mkubwa wa michezo Msoga, Chalinze Mkoani Pwani.
"Hii ni kama shukrani yetu kwa utumishi wa Rais wa awamu ya nne Dk. Jakaya Kikwete, mengi tumeyapa majina Kikwete lakini sio Msoga, hapa hatukufanya kitu kwahiyo uwanja ule tutauweka Msoga kuonesha shukrani yetu kwa Rais wa awamu ya nne," amesema Dk. Samia.
Dk. Samia ameyaeleza hayo leo Jumapili Septemba 28, 2025 wakati wa kampeni zake kwenye eneo la Msoga mkoani humo akiwa njiani kuelekea Mkoani Tanga.
Pia ameahidi kuendelea kusogeza huduma za kijamii karibu zaidi na wananchi pamoja na kuendelea na uhakiki wa madai ya fidia kwa baadhi ya wananchi wa Msata waliopisha miradi ya maendeleo kwenye eneo hilo.