Msimu uliopita ndio mkataba wangu na Asec Mimosas ulifika ukingoni, mabosi waliniita mezani tukazungumza na tukafikia uamuzi wa kuongeza kandarasi.
Siwezi zungumzia sana hatima yangu ndani ya Asec kwasasa kisa mchezo mmoja na ikitokea hivyo maamuzi yote yatafanywa na management yangu ila kiufupi huu ndio wakati sahihi wa kuanza kuwaza kuhusu hilo"
"Majuto ni makubwa kwasababu tulitakiwa kumaliza huu mchezo ugenini siku yakwanza lakini tumeshindwa kufanya hivyo na leo tumetolewa CAFCL katika hatua za mwanzo kabisa..
Kama nitaendelea kusalia Asec naamini bado nina mambo mengi makubwa ya kufanya ana moja yapo ni kuhakikisha tunatwaa makombe yote ya ndani kwa msimu huu."
Ikumbukwe kocha huyu alikuwa akihusishwa kujiunga na Yanga kama kocha mkuu huku Roman Folz akiwa msaidizi na baadaye akaitosa Yanga na kusalia ASEC jambo ambalo liliwachanganya mabosi wa Yanga, sasa anafikiria kuondoka