Klabu ya Asec Mimosas ya Ivory Coast imesukumizwa nje ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kufuatia kipigo cha penalti 5-4 baada ya sare ya jumla 1-1 dhidi ya Power Dynamos ya Zambia kwenye hatua ya awali.
Power Dynamos itachuana na vigogo wa Uganda, Vipers Sc kwenye raundi ya pili ambapo miamba hiyo ya Zambia itaanzia ugenini, Kitende, Uganda kati ya Oktoba 17-19, 2025 na kurudiana kati ya nyumbani Zambia kati ya Oktoba 24-26, 2025.