Kutokana na ratiba ilivyobana, mchezo wetu wa nyumbani dhidi ya Mashujaa FC utafanyika Septemba 30 jijini Dar es Salaam, kwenye Uwanja wa KMC saa 10:00 jioni.
Uamuzi huu umefikiwa ili kuwapa wachezaji muda wa kupumzika na kujiandaa vyema, hasa baada ya mchezo mgumu wa jana wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Rayon Sports.
Baada ya mchezo huo, tutakuwa tumemaliza rasmi ratiba ya mwezi Septemba na timu itarejea nyumbani Singida kwa maandalizi ya michezo ijayo, amesema Hussein Masanza msemaji wa Singida Black Stars