RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amemzawadia nyumba Mwanariadha wa mbio ndefu, Alphonce Felix Simbu Jijini Dodoma kufuatia Sajinitaji huyo wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kushinda Medali ya Dhahabu kwenye Mashindano ya Dunia wiki mbili zilizopita.
Hayo yamelezwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa katika hafla ya kumpongeza mwanariadha huyo leo Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam baada ya kushinda ubingwa wa Dunia wa Marathon Jijini Tokyo nchini Japan Septemba 15.
Pamoja na zawadi ya nyumba, Waziri Mkuu, Majaliwa amemkabidhi Simbu hundi yenye thamani ya Shilingi Milioni 20 ambayo ni zawadi kutoka Baraza la Michezo la Taifa (BMT).
Awali, akizungumza kwenye hafla hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dk. Samia ina mchango kubwa katika sekta ya michezo.
Amesema hivi sasa wamejipanga kuhakikisha Tanzania inashinda tena Medali kwenye Mashindano yajayo ya Jumuiya ya Madola mwaka 2026 na Mchezo ya Olimpiki mwaka 2028