BAADA ya kucheza na Mbeya City kwenye mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu Bara Tanzania akiwa na Azam FC; Kocha Florent Ibenge amefunguka kuwa ameshaona Ligi ya Bongo ni moja ya Ligi ngumu zaidi barani Afrika.
"Si rahisi. Michezo si rahisi, nadhani michuano hii (NBCPL) ni moja ya michuano migumu zaidi barani Afrika. Kwahio tunapaswa kuchukua alama kwa kila mchezo." Alisema Ibenge.
Akiongeza kuwa changamoto alizoziona zinamfanya atafute mbinu zaidi za kuliboresha kundi lake kwani hajaridhika na kiwango cha wachezaji.