Yusuf Kagoma (29) atakosa mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Gaborone United baada ya kuumia mguu wa kulia.
Kagoma aliumia kipindi cha kwanza cha mchezo wa jana dhidi ya Fountain Gates, akaendelea kucheza kwa muda lakini alilazimika kutolewa mapema kipindi cha pili. Uchunguzi umeonyesha jeraha lake ni kubwa kuliko ilivyodhaniwa awali, hivyo hatakuwa sehemu ya kikosi cha marudiano.
Simba SC itamkosa mchezaji muhimu katika mchezo huu wa kuamua hatma yao kwenye ligi ya mabingwa.