TIMU ya KMKM imefanikiwa kuingia Hatua ya Timu 32 ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya AS Port ya Djibouti leo katika mchezo wa marudiano wa Raundi ya Kwanza ya leo Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
Kwa matokeo hayo, KMKM inakwenda Raundi ya Pili kwa ushindi wa jumla wa 4-2 kufuatia ushindi mwingine wa 2-1 kwenye mchezo wa kwanza wiki iliyopita hapo hapo New Amaan Complex.
Sasa KMKM itakutana na mshindi wa jumla kati ya Azam FC na Al Merreikh FC Benteu, maarufu kama Al Merreikh Juba ya Sudan Kusini.
Azam FC ipo kwenye nafasi nzuri ya kusonga mbele baada ya ushindi wa 2-0 kwenye mchezo wa kwanza na Al Merreikh FC Benteu mjini Juba nchini Sudan Kusini na timu hizo zitarudiana Jumapili Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.