MASAU BWIRE ADAI STARS INA USIMBA NA UYANGA
Na Shafih Matuwa
MSEMAJI wa timu ya JKT Tanzania, Masau Bwire amedai tatizo la timu ya taifa, Taifa Stars ambalo linaitafuna siku hadi siku ni kuwa na Usimba na Uyanga kila ambapo inateuliwa kushiriki mashindano.
Bwire ameyasema jana mara baada ya timu ya taifa, Taifa Stars kuondoshwa kwenye michuano ya mataifa Afrika, AFCON inayoendelea nchini Ivory Coast.
Msemaji huyo aliyepata umaarufu akiwa na Ruvu Shooting iliyoshuka daraja, amesema timu hiyo imejaa Usimba na Uyanga na kama tabia ikiendelea itakuwa ngumu kukubalika na watu wengine wasiozipenda timu hizo