BABACAR SARR ATABIRIWA MAKUBWA SIMBA
Kocha wa viungo wa timu ya Al Nassr ya Saudi Arabia, Junior Robertinho ambaye ni mtoto wa aliyekuwa kocha wa Simba, Robertinho Oliviera amesema kiungo mpya wa Msimbazi, Babacar Sarr ni mtu wa kazi
Sarr aliyesajiliwa msimu huu kutoka US Monastir tayari amecheza mechi mbili, kwani
aliposajiliwa tu alikuta timu ikiwania ubingwa wa Kombe la Mapinduzi Zanzibar.
Japokuwa Wekundu hao hawakutwaa kombe hilo mbele ya mabingwa watetezi Mlandege, Sarr ni miongoni mwa wachezaji
walioingia kipindi cha pili walipocheza dhidi ya Singida Fountain Gate, na fainali kocha
alimpanga kikosi cha kwanza ingawa inaonekana bado kuna mashabiki hawajamuelewa
Junior amesema amewahi kumuona kiungo huyo kwa muda wa dakika 90 walipocheza na US Monastir na alikuwa mchezaji hatari.
Alieleza kuwa, hakuna mchezaji ambaye hana matokeo kwenye timu halafu akachezeshwa mechi nzima na hiyo tu inaonyesha ni aina gani ya mchezaji Simba
wamempata.
"Niliwasikia makocha wake wakisema ni mchezaji mwenye nidhamu ya ukabaji na
tulipocheza nao alikuwa na utulivu mkubwa uwanjani na kupokonya mipira kwa haraka hasa kwenye kufungua njia za kupitisha mipira," alisema
Aliongeza kuwa kipaji chake kinaweza kuisaidia Simba ambayo alikuwa anaiona muda mrefu wakati baba yake alipoifundisha kuhitaji mtu mwenye uwezo wa kurudisha ugumu kwa timu pinzani uwasogelea mabeki wa kati.
"Baba yangu alikuwa ananiambia Tanzania soka lao linatumia nguvu Sana. Pengine hilo ndilo eneo ambalo Sarr anatakiwa ajipange nalo, kwani timu aliyotoka alikuwa ni kiungo mstaarabu hakUwa na matumizi makubwa ya nguvu"
Sarr anaonekana kuwa na kazi ya ziada ndani ya timu hiyo, kwani wachezaji anaocheza nao nafasi moja tayari walishaonyesha makali mbele ya kocha Abdelhak Benchikha na wanafahamiana namna ya uchezaji
Viungo anaocheza nao ni Mzamiru Yasin, Fabrice Ngoma, Sadio Kanoute na Abdallah
Hamisi