JOSEPH GUEDE KUTUA WIKI HII
Wiki hii mshambuliaji mpya wa Yanga Joseph Guede anatarajiwa kutua nchini kuungana na wenzake ambao wanaendelea na
mazoezi Avic Town kujiandaa na mechi za Ligi Kuu, kombe la FA na Ligi ya Mabingwa
Baada ya kukamilisha usajili wake, Guede alipewa ruhusa maalum ili akamilishe masuala binafsi kabla ya kutua nchini kuanza majukumu mapya na mabingwa hao wa nchi
Yanga inarejea mazoezini leo baada ya mapumziko ya mwishoni mwa wiki ambapo wiki hii vijana wa Kocha Miguel Gamondi wanatarajia kucheza mechi kadhaa za kirafiki
Katika moja ya mahojiano yake, Gamondi alisema amemuagiza Guede akatishe mapumziko na kutua nchini haraka ili aanze
mazoezi na wenzake
Gamondi alisema Guede anatakiwa kuja kufanya maandalizi haraka na wenzake ambayo yatamrahisishia kuwa na mwanzo mzuri ndani ya timu hiyo wakati wa mashindano utakaporejea
"Tunaendelea na mazoezi yetu, wikiendi tulipumzika kidogo kazi zaidi itaendelea Jumatatu ni muhimu kuwa tayari mapema
nafurahia jinsi wachezaji wanavyojituma licha ya ugumu wa ratiba ya mazoezi"
"Kwa sasa kila mchezaji ambaye hayupo a timu ya taifa tupo naye kasoro kijana wetu Guede. Nimeongea naye nimemwambia
"Anahitaji kuanzia hapa ambako tunafanya sasa ili imsaidie kuwa sawa na wenzake, naamini atafika kama ambayo tumezungumza,
hatuna shida sana na hawa ambao wako timu za taifa kwa kuwa wao wanapata mazoezi ya
kutosha," alisema Gamondi