GIFT FRED APEWA NAFASI NYINGINE NA GAMONDI
Mlinzi wa kati wa Yanga Gift Fred raia wa Uganda amepewa nafasi nyingine ya kupigarnia nafasi yake katika kikosi cha kwanza
Gift aliyetua Yanga katika dirisha kubwa la usajili lililopita akitokea SC Villa ya Uganda, alimanusra apewe mkono Wa kwaheri katika
usajili wa dirisha dogo
Hata hivyo kiwango alichoonyesha katika michuano ya kombe la Mapinduzi kikabadili
upepo kwani Kocha Miguel Gamondi akapendekeza Mganda huyo aendelee kusalia katika kikosi chake
Ni wazi bado atakuwa na kazi ya kupigania nafasi yake mbele ya nahodha Bakari Nondo
Mwamnyeto, Ibrahim Bacca na Dickson Job
Wakati yeye akiendelea na mazoezi Avic Town, wenzake wako kwenye majukumu ya timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars' wakishiriki michuano ya Afcon 2023.
Hatma ya Tanzania kuendelea kubaki lvory Coast au kurejea nchini itaamuliwa Leo kwenye
mchezo wa tatu hatua ya makundi dhidi ya DR Congo
Tanzania inahitaji kushinda mchezo huo ili kukata tiketi ya hatua ya mtoano