IVORY COAST YAMUOMBA KOCHA WA WANAWAKE UFARANSA AWAFUNDISHE KWA MUDA AFCON

Imeripotiwa kuwa Shirikisho la soka nchini Ivory Coast limewasilisha ombi kwa Shirikisho la soka nchini Ufaransa la kutaka kumuazima kwa mkopo kocha wa timu ya taifa ya wanawake ya Ufaransa, Hervé Renard (55) kwa ajili ya kuja kuifundisha timu ya taifa ya Ivory Coast kwa muda hadi pale michuano ya AFCON itakapomalizika.

Hervé Renard amewahi kuiongoza Ivory Coast kwenye michuano ya AFCON mwaka 2015 na kufanikiwa kutwaa kombe hilo, kwa Sasa Herve Renard ni Kocha mkuu wa Timu ya Taifa ya Wanawake wa Ufaransa, ikumbukwe Kocha huyo ameshawahi kutwaa mataji mawili ya AFCON akiwa na Zambia Chipolopolo


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA