MUSONDA KUREJEA YANGA NA MOTO WA AFCON
Mshambuliaji wa Yanga Kennedy Musonda alikuwa na wakati mzuri kwenye michuano ya Afcon 2023 akiwa na kikosi cha timu ya Taifa
ya Zambia
Musonda alipata nafasi ya kucheza katika kikosi cha kocha Avram Grant akianzishwa katika mchezo wa mwisho dhidi ya Morocco, mchezo uliohitimisha ushiriki wa Zambia baada ya kipigo cha bao 1-0
Ni wazi michuano hiyo imemuongezea Musonda ari, morali na kujiamini. Pengine
Wananchi watarajie kuona analeta kasi hiyo katika ligi kuu ya NBC
Yanga imeongeza ushindani eneo la ushambuliaji baada ya kumsajili Joseph Guedo katika dirisha dogo