CAPE VERDE KUMNGOJA SENEGAL AU IVORY COAST
Bao pekee lililofungwa na nahodha wa timu ya taifa ya Cape Verde, Mendez limeiwezesha kutinga robo fainali baada ya kuilaza Maurtania bao 1-0 kwenye mchezo uliomalizika muda huu hatua ya 16 bora Afcon zinazofanyika Ivory Coast.
Jana usiku DR Congo iliifuata Guinea baada ya kuiondosha kwa matuta Misri baada ya sare ya 1-1 ndani ya dakika 120, DR Congo ilipata penelti 9 dhidi ya 8 za Misri.
Mechi itakayofuata usiku huu ni kati ya wenyeji Ivory Coast na mabingwa watetezi Senegal