MGOSI AIANGUKIA TFF

Kocha Msaidizi wa Simba Queens, Mussa Hassan ‘Mgosi’ ameliomba Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuangalia uwezekano wa kurekebisha ratiba ya ligi hiyo kutokana na kupitia changamoto mbalimbali zinazowasababishia kukosa muda wa kupumzika.
.
“Tumetoka Dar kwenye mechi na JKT Queens, tukasafiri kwenda Iringa kucheza na Amani, kisha Musoma dhidi ya Bunda halafu tumecheza tena Dar na Bunda kisha tutarudi tena Dodoma hivyo kuna haja ya TFF kuangalia hilo,” alisema na kuongeza;
.
“Licha ya changamoto hiyo ila sisi bado tunaendelea na mapambano yetu ili tufanye vizuri na kuchukua ubingwa kwa msimu huu.” Timu hiyo inaendelea kushika nafasi ya pili baada ya michezo ya raundi ya sita huku JKT Queens ikiendelea kuongoza na pointi 18.
.
Musa Mgosi kocha msaidizi Simba Queens

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA