DITRAM NCHIMBI AIBUKIA LIGI KUU RWANDA
Nyota wa zamani wa Polisi Tanzania, Young Africans na Taifa Stars Ditram Nchimbi 'Duma' amejiunga na Klabu ya Etincelles FC inayoshiriki Ligi Kuu nchini Rwanda kwa mkataba wa nusu msimu hadi June 2024.
Mshambuliaji huyo anajiunga na Etincelles Club kama mchezaji huru baada ya kusitishwa kwa mkataba wake na FGA Talents FC ya Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara, Nchimbi amewahi kutamba pia na Vilabu vya Majimaji FC, Mbeya City, Njombe Mji na Polisi Tanzania.