YANGA KUIVAA HOUSING FC FA CUP
Baada ya takribani mwezi mzima kwa mashabiki wa Yanga kukosa burudani ya timu yao, hakuna tena muda wa kusubiri kwani
keshokutwa Jumanne, Januari 30 Yanga itakuwa uwanjani kumenyana na Housing Fc katika mchezo wa kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) raundi ya pili
Yanga tayari imeweka hadharani vingilio vya mchezo huo ambapo VIP A ni Tsh 20,000/-, VIP B ni Tsh 10,000/- na Mzunguuko ni Tsh 5,000/-
Mtanange utapigwa saa 1 usiku Katika Uwanja Wa Azam Complex Chamazi