MAMELOD YANASA KIUNGO WA ORLANDO PIRATES
Klabu ya Mamelodi Sundowns FC imekamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji Thembinkosi Lorch (30) kutoka Orlando Pirates FC, Lorch aliyeitumikia Pirates kwa miaka 8 akicheza michezo 176, akifunga magoli 34.
Huu Unakuwa Usajili wa nne kwa "Masandawana" katika dirisha ili Usajili mwezi Januari baada ya kuwasajili Tashreeq Mathew kutoka IK Sirius ya Sweden, Matias Esquivel kutoka Club Atletico Lanus ya Argentina na Zuko Mdunyelwa kutoka Chippa United.